Nigeria yajiliwaza na nafasi ya tatu #Afcon2019
Alhamisi, Julai 18, 2019
Nigeria yajiliwaza na nafasi ya tatu #Afcon2019

Timu ya Taifa ya Nigeria imetwaa nafasi ya tatu katika michuano ya #Afcon2019 baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya dhidi ya Tunisia usiku wa kuamkia leo.

Katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Al- Salam wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 30,000 kwa wakati mmoja, jijini Cairo, goli la mapema lililowekwa kimiani na Odion Ighalo katika dakika ya tatu lilitosha kabisa kuipa Eagles nafasi hiyo ya tatu.

Hii ni mara ya nane kwa Nigeria kushika nafasi ya tatu katika mashindano hayo makubwa zaidi Barani Afrika. Kikosi cha tai hao wa Nigeria kiliongozwa na nahodha wao, John Obi, Mikaeli anaye kipiga katika klabu ya Trabzonspor nchini Uturuki, Odion Ighalo, Ahmed Musa, Alex Iwobi na Samueli Chukwueze.

Gazeti la Habari Leo.