NIGERIA, ALGERIA WASAKA KUCHEZA FAINALI
Jumamosi, Julai 13, 2019
NIGERIA, ALGERIA WASAKA KUCHEZA FAINALI

NIGERIA na Algeria zitachuana katika mpambano wa kusaka nafasi ya kucheza fainali ya michuano ya 32 ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) wakati watakapokutana katika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo kesho Jumapili Julai 14.

Nigeria imepata nafasi hiyo ya kucheza nusu fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Afrika Kusini. Super Eagles iliifunga Bafana Bafana, shukrani kwa mabao ya Samuel Chukwueze na William Troost-Ekong. Mbinu za kiufundi za kocha Gernot Rohr zilidhihirisha ubora dhidi ya zile za Afrika Kusini, huku kiungo wa Afrika Kusini akitawala mchezo huo. Wasiwasi pekee ulikuwa kwa mshambuliaji Odion Ighalo, ambaye alikuwa akicheza mashindano hayo kwa mara ya kwanza.

Hatahivyo, ilikuwa jukumu la mabeki wawili wa kati wa Bafana Bafana ambao waliwawezesha mabeki wa kati kuwaruhusu washambuliaji wa pembeni Ahmed Musa na Chukwueze, pamoja na mchezeshaji Alex Iwobi, kung’ara.

Wakati huohuo, Algeria walifanya kweli mbele ya Ivory Coast na kushinda kwa penalti juzi usiku. Algeria inacheza nufu fainali ya kwanza tangu mwaka 2010 na inaangalia kurejea katika fainali kwa mara ya kwanza tangu ilipotwaa ubingwa kwa mara ya kwanza mwaka 1990 ilipokuwa mwenyeji wa mashidano hayo.

Gazeti la Habari Leo