KOCHA MADAGASCAR ATOA NENO
Jumamosi, Julai 13, 2019
KOCHA MADAGASCAR ATOA NENO

KOCHA wa timu ya taifa ya Madagascar, Nicolas Dupuis amesema ni vigumu kwa timu inayoshiriki kwa mara ya kwanza fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) na kufikia robo fainali, kufanya vizuri katika mashindano yajayo.

 Timu hiyo kutoka katika visiwa vya Bahari ya Hindi ilishuhudia ndoto zao zikiyeyuka baada ya juzi Alhamisi kufungwa 3-0 na Tunisia, nchi iliyopo katika nafasi ya 83 juu yake katika viwango vya Fifa. “Ninajivunia kile ambacho wachezaji wangu wamekifanya, tangu kuanza kwa mashindano haya. Kwa kweli nimewavulia koa, “alisema Dupuis, ambaye mkataba wake ulitarajia kumalizika wakati wa mashindano hayo nchini Misri.

 “Leo hatua ni kubwa sana. Kuhusu hatma yangu, hilo halijalishi sana. Nimekuwa mwenye heshima kubwa na kipambule change ni Madagascar.” Dupuis alianza kuifundisha Madagascar mwaka 2017 na kuibadili timu hiyo ya taifa ambayo ilikuwa katika nafasi ya 190, na kufanya vizuri katika mechi za kufuzu kwa ajili ya mashindano hayo na kutoa mshangao kwa kufuzu kwa mashindano hayo. “Sijui kipaumbele cha Magascar kwa upande wa kunibakisha mimi, “aliendelea kusema Dupuis. Itakuwa ngumu zaidi kipindi kijacho. Kuna kazi nyingi za kufanya Madagascar.

“Tunatakiwa kuendelea kucheza, tunatakiwa kurudi nyumbani na kufanya kazi.” “Kwa kweli sijutii kwa lolote, “aliongeza kocha huyo. “Tulikuwa juu dhidi ya timu kubwa.”

Gazeti  la Habari  Leo