Haya ndio maajabu ya fainali za Kombe la Afrika
Jumanne, Julai 23, 2019
Haya ndio maajabu ya fainali za Kombe la Afrika

. Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka huu zimefikia tamati nchini Misri, juzi Ijumaa ambapo Algeria imemaliza ikiwa bingwa, baada ya kuichapa Senegal bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali.

Ushindi huo dhidi ya Senegal unaifanya Algeria iwe imetwaa taji hilo mara mbili, ubingwa wa kwanza ikichukua mnamo mwaka 1990 wakati fainali hizo zilipofanyika nchini mwao.

Mbali na Algeria kutwaa ubingwa, kumekuwa na timu, wachezaji na waamuzi waliofanya vyema kwenye vipengele mbalimbali lakini wapo ambao wamechemsha katika mashindano hayo ya mwaka huu kutokana na sababu moja au nyingine.

Tathmini ya jumla ya mashindano ya Afcon za mwaka huu kwa kuainisha vinara na waliochemsha kwenye vipengele mbalimbali na kuainisha takwimu na badhi ya rekodi zilizowekwa kwenye mashindano hayo mwaka huu.

Mchezaji Bora-Ismael Bennacer (Algeria)

Kiungo wa Algeria mwenye umri wa miaka 21, Ismaer Bennacer ameibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mashindano ya Afcon mwaka huu kutokana na kiwango bora alichoonyesha katika fainali hizo.

Gazeti la Mwanaspoti.